Curriculum
Course: usimamizi wa fedha
Login
Text lesson

2. Usitumie zaidi ya ulichonacho

Je, umeshaanza kufuatilia kwa karibu kipato na matumizi yako? Kuna mshangao wowote? Je, ubainishaji wa matumizi yako hukufanya ufikiri kabla ya kutumia? Sasa unaweza kupata hali halisi ya kipato chako na kile unachotumia, hebu tuipitie kanuni nambari moja: Mizania (Kiasi). 

Usitumie zaidi ya ulichonancho. Gharama za matumizi yako ni lazima  zisizidi kipato chako…maelezo mengine zaidi (yapo katika somo la 3)!
Lakini jambo hili huonekana gumu kuliko inavyofikiriwa. Kwa nini? Hii ni kuwa changamoto kubwa ni kwamba mara zote gharama za matumizi na mapato kila moja huja kwa wakati wake tofauti. Kwa mfano, tunapata kipato cha mara moja au mbili kwa mwezi … lakini baadhi ya gharama za matumizi yetu ni za kila siku, au baadhi ni za kila mwaka.

Na mara zote bongo zetu wanadamu hujishughulisha na namna ya kutunza ama kusimamia muda vizuri: Fikiri kuhusu hilo…ni watu wangapi ni mawakili wa muda? Na je, ni miradi mingapi huanzishwa na kukamilika kama ilivyopangwa?  

Hatuwezi kusahau mahitaji ya kila siku…kama chakula au usafiri. Lakini tunasahau mahitaji yasiyohitajika mara kwa mara, kama vile ada ya shule ambayo hulipwa kwa mwaka, au kodi ya mapato ambayo hulipwa kwa mwaka. Fikra zetu zimelenga katika mahitaji ya muda mfupi zaidi. Na kama tunajua kuwa kuna gharama nyingi zitatokea usoni…mfano likizo, sherehe za kifamilia…ama kustaafu…ni vigumu kuingiza gharama hizo zote katika mapato yetu…bila ya kuathiri mizania. Inahitaji kufikiri kwa hali ya juu!

Zoezi la Nyumbani:

  1. Angalia mizania yako: Angalia ufuatiliaji wako: Je, gharama za matumizi zinalingana na mapato yako? Usitumie zaidi ya ulichonacho! 
  2. Orodhesha matumizi yako yote ya kila mwaka ama yasiyohitajika mara kwa mara-hii ni pamoja na matumizi ya baadae ama ya muda mrefu unayokusudia kufafanya, yaweza kuwa(harusi? Marekebisho ya nyumba yako? Safari?…).

 

Mazoezi:

  1. Orodhesha gharama zote za matumizi yako ambazo si za kila siku, kama vile kodi ya nyumba, ada za shule, likizo, kodi ya mapato ya kila mwaka, n.k… 
  2. Mara nyingi gharama za matumizi hazifanani. Hivyo ni vyema kufikiri kwa kina ni aina gani ya gharama hizi: hii itakusaidia kuweka kipaumbele…kwa sababu orodha ya mahitaji siku zote ni ndefu sana! 
    1. Matumizi ya Lazima: Mfano umetoa ahadi, umeingia mkataba: yakupasa kulipa. 
    2. Lengo: Jambo fulani ungependa kulifanya, mfano maboresho ya nyumba, au zawadi kwa mtoto.  
    3. Wajibu” kama vile likizo, au kuhudumia familia…gharama ambazo unajisikia kuwajibika kimaadili kwa familia yako au nduguzo ama marafiki zako.  Kwa mfano, gharama za chuo kikuu kwa ajili ya mtoto wako inaweza kuangukia katika “wajibu” lakini ada za shule ndani ya mwaka husika inaweza kuangukia katika “matumizi ya lazima”…wakati kusomea shahada kwa ajili yako inaweza kuwa ni “lengo”.
  3. Uwiano: hii itakusaidia kufanya mahesabu ya kiasi gani unahitaji kuweka akiba kila mwezi kwa ajili ya gharama za matumizi fulani: kwa mfano, ikiwa gharama zake ni za mara moja kwa mwezi, andika “1”; ikiwa ni mara moja kwa mwaka, andika “12” (lazima uweke akiba sehemu ya kumi na mbili kwa kila mwezi), ikiwa ni katika miezi mitano, andika “5”, n.k. Kumbuka: kwa mfano, malipo ya ada ya shule hufanyika mara moja kwa kila mwaka katika mwezi wa Septemba na wakati huo tupo katika mwezi wa Mei. Na ikiwa umekuwa ukiweka akiba kwa miezi yote, andika “12”. Lakini ikiwa haujaweka akiba yoyote kwa miezi yote, andika “3” (una miezi mitatu tu kuweka akiba kwa kiasi chote cha ada).  
  4. Ongeza: Sehemu hii orodhesha mahitaji yako yote na uweke  vipaumbele kulingana na uwekaji wa akiba zako wakati huo huo ukizingatia mizania ya kipato chako (wewe bado unahitaji kula, kuoga, kusafiri…).