Curriculum
Course: usimamizi wa fedha
Login
Text lesson

5. Zingatia kilicho muhimu

Punguza uchaguzi, panua fikra: fanya vitu vichache, kwa tija. 

Wiki iliyopita, tulichambua kwa makini juu ya aina mbili za matumizi: yale unayoweza kuyasimamia/kuyadhiti na ambayo umeahidi kuyatekeleza.

Lakini kwa yale tunayoweza kuyadhibiti…mara nyingi yanakuwa nje ya udhibiti wetu! Swali: ni kipi kilichokigumu kudhibiti? Pochi zetu za fedha ama mawazo yetu? 

Leo tunaangazia juu ya bongo zetu na jinsi tunavyo fanya maamuzi. Unaweza kujaribu jaribio hili kila asubuhi kwa kunywa maji ya matunda, kwa kiasi sawa. Kisha kwa siku moja nyingine, unakunywa nyingi zaidi.

Je, utakoma baada ya kunywa tofauti na kawaida yako? Inawezekana ukaendelea kunywa hata bila ya wewe kutambua. Hii ni sawa kabisa  na kutumia vipato vyetu. Kama tunapata vipato vikubwa zaidi, kwanini tunajikuta tumetumia chote? 

Bongo zetu huzingatia zaidi vitu vya muda mfupi: na hii ni rahisi zaidi. Kwani inahitaji nguvu zaidi kufikiria vitu vya muda mrefu. Hivyo wengi wetu hatupendi kujisumbua katika kufanya hilo. Maamuzi yetu mengi ni kwa hisia,… kwa sababu inahitaji nguvu zaidi kufikiri mambo yakinifu. Ni aina gani ya maamuzi ya fedha hutokana na mawazo mafupi yatokanayo na hisia? 1)kutumia kipato chote ulicho nacho. 2) Kununua kwanza vitu tunavyovipenda huku tukisahau vitu vya msingi ambavyo hata matumizi yake ni madogo…na kuingia katika shida ama hofu pindi tunapogundua kuwa hatuna pesa tena.

Tunawezaje kuzifanya bongo zetu kufikiria vitu vya muda mrefu na vyenye mantiki zaidi? 

Tumeshakwisha anza tayari: Orodha hii yote (gharama za matumizi ya baadaye, kulipa madeni) hutusaidia kukumbuka malengo ya muda mrefu…kwa kuorodhesha manunuzi ya dukani na kuyazingatia ama kutunza orodha ya mahitaji yetu katika pochi zetu inasaidia sana pia. Kuweka ukomo kama vile kufanya mahesabu ya ukomo wa matumizi ya siku ama kwa kutumia bahasha au kwa kubeba kiasi kidogo cha fedha katika pochi zetu inasaidia kwa kiasi kupunguza matumizi tunayo yafanya kwa hisia bila maamuzi sahihi. Kwa kufanya ufuatiliaji wa kila tunachofanya, inatusukuma kufikiri kwa kina juu ya nini tunatumia fedha zetu.  

Wiki ijayo, tutaangalia utengenezaji wa bajeti ambayo itatusaidia kufikiri mambo ya muda mrefu na kuweka ukomo wa matumizi yetu.

Tunaweza kwenda mbele zaidi ya hapa … kutoka kufikiria malengo ya muda mrefu na kufanya fikira yakinifu na kuwa makini na wenye busara zaidi juu ya maisha yetu ya kifedha. Tunapo nunua, tunazingatia tu vitu (au huduma)tunavyonunua. Ninunue nini? Tunapojadiliana na marafiki zetu, tunauliza: Umenunua nini? Matumizi ya wanajamii wenzetu hutufanya kuwa watumwa katika kuamua “kipi”…ama “vipi” vitu hivi ni kama sukari – hutufanya kuhitaji kila mara na kamwe hatutosheki. Kwa hiyo tunapoona kitu kipya, tunakitaka, na hata kile pia,  na kile “nini” kama vile … yamkini hili sio swali sahihi kwani kamwe halijawahi kupatiwa jawabu la kuridhisha. 

Na kama tutaweka mbada wa swali “nini” kwa “kwanini”? kwanini ninunue hiki? Kulisha mwili wangu, ili niwe na afya, n.k…na yatupasa kufikiri kama hakuna sababu, kwani inaweza kuwa ikawa haina faida kabisa maishani mwetu na ikawa na mbadala wake katika kutumia fedha zetu (na “kwanini”) Hii ni hatua ya kwanza ya kuwa mwangalifu: kitu chochote unachonunua ama tumia, fikiria “kwanini” na sio “nini”. Hii pia husaidia kuoanisha maisha yetu na yale ya kifedha: tunatumia au kununua au kuweka akiba au kutoa kwasababu maalumu, kwa sababu inatija maishani mwetu. Na zaidi tujiulize wenyewe “kwanini”, zaidi huondoa msuguano katika maisha yetu kati ya tabia za matumizi yetu na maadili yetu ya kimaisha.

Tunavyozidi kuwa makinifu katika usimamizi wa fedha zetu, huibua maswali mengine katika bongo zetu:  kuwa tunanunua vitu hivi…vinatoka wapi? Nani kavitengeneza? Manunuzi yetu hutuunganisha na wanadamu walio vitengeneza, safirisha, viuza na mahali vitokako. Vitu huwa na thamani zaidi na tunasita kuviharibu na kununua toleo jipya-ama ungeweza kuufuta mchoro wa mtoto wako? Mapatano mazuri…huonekana tofauti tunapojaribu kuona jinsi bei inavyo athiri wengine. Badala ya kununua vitatu (Huonekana ni nafuu), tunaweza kupendelea vitu vilivyotengenezwa kienyeji katika karakana ambapo wafanyakazi huheshimiwa na kulipwa mshahara mzuri; inaweza kuwa ghali zaidi, lakini tunakuwa na uhakika ni wapi fedha zetu zinaenda. Kwa nini … na sio “nini”, hutufanya kuishi kama binadamu kamili, na si tu watumiaji wa vitu.

Punguza uchaguzi, panua fikra: fanya vitu vichache, kwa tija. 

Mazoezi

Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia katika kuwa mtu mwenye matumizi yakinifu. Inategemea pia na mwenendo wa matumizi yako na nini unakithamini zaidi.  

  1. Jitambue: kama umekwisha jaribu  jaribio la maji ya matunda, unaweza jaribu njia zingine ili ugundue jinsi bongo zetu hufanya maamuzi. Kwa mfano unapakua kiasi sawa katika sahani ama bakuli kwa muda wa siku kadhaa. Kisha unaweka kiasi sawa katika bakuli kubwa au sahani: Hauoni inakuwa ni kiasi kidogo? Na pia inaonekana pungufu baada ya kula? Unapofahamu zaidi jinsi ubongo wako unavyofanya kazi, hukufanya kujitambua unavyoweza kuwa     “kudanganyika” au kupata msukumo unaponunua. Wenye maduka na watafuta masoko wanafahamu mahitaji ya ubongo wako zaidi yako mwenyewe. Na kama ukitaka kujifunza zaidi, vitabu hivi viwili vinaeleza vizuri katika mada hiyo:
    1. Jinsi Tunavyoamua, Yona Lehrer
    2. Kufikiri, haraka na Taratibu, Daniel Kahneman
  2. Acha, Fikiri, Amua: kila unapotaka kutumia pesa, usiharakishe: Vuta pumzi kwanza, tulia, fikiri…kwanini? na sio nini? Ni kwa jinsi gani gharama hizo zitaweza kubadili maisha yako? 
  3. Punguza uchaguzi: Orodhesha manunuzi yako ukiwa nyumbani, kisha uyazingatie. 
  4. Bahasha: kama muda mwingi unatumia pesa tathilimu, angalia ni kiasi gani umeamua kutumia. Kwa mfano katika chakula, au vitabu, au kwa ajili ya matembezi (gharama yoyote ambayo unaona ni vigumu kuidhibiti mwenyewe) weka kiasi katika bahasha tofauti na uiandike “chakula”, “vitabu” n.k…na utumie tu kiasi kilichopo katika bahasha hiyo. 
  5. Soma alama za maelekezo: Ni wapi bidhaa hiyo inatoka? Imetengenezwa na Kampuni gani? Pata taarifa zaidi.
  6. Orodhesha tunu za maisha yako: Je, matumizi yako yanaendana na tunu zako? Kwa mfano, kama unathamini elimu kama moja ya tunu zako muhimu, na unatambua umetumia zaidi kwa kununua nguo badala ya vitabu, unaweza hisi kuchanganyikiwa.
  7. Fuatilia: Unafahamu unatumia juu ya nini…jaribu kuangalia ni kwa nani fedha zinaishia.