Habari yako? Je, umeshaanza kukitekeleza kile ulichojifunza katika kozi hii? Tayari umeshafanya nusu ya masomo na kujifunza zana kuu katika kusimamia fedha: Ufuatiliaji, kupanga (bajeti), kuorodhesha gharama za matumizi ya baadaye (ahadi/vitu vya lazima na miradi) na kuweka akiba kwa ajili yake, kuweka kipaumbele katika gharama za matumizi na kuweka ukomo wa matumizi, kupunguza hatari…zana hizo zote hutusaidia katika usimamizi wa fedha wenyewe kwa kujiwekea kikomo na vitu vya kutukumbusha, vinavyoonyesha ni vitu gani tumefanya na wapi tunaelekea.
Tungelipenda kukomea hapa…lakini kuna changamoto kubwa moja: hatuko peke yetu katika usimamizi wa fedha. Katika nusu ya pili ya kozi hii, tutangalia fedha na mambo mengine…mwenzi ambaye hutumia fedha kwa vipaumbele tofauti, watoto ambao huliilio midori, ndugu ambao huhitaji msaada, majirani, jamii, jiji, nchi…tutaweza kuongeza uwanja wa mjadariano kwa wakati mmoja na hii itatusaidia kuangazia mada zingine kama vile uwekezaji, kustaafu na uwekaji benki kwa njia tofauti: fedha ni chombo cha kijamii.
Hebu tuanze na sehemu ndogo ya jamii: familia – hasa mwenzi. Kama haujaolewa bado, soma somo hili kama “kinga”…na kama tayari umekwisha olewa, soma kama “tiba”!
Kutoka katika Uadui hadi Ushirikiano: vita dhidi ya Ushirikiano.
- Kubishana juu ya fedha ni mara kwa mara, katika familia zote, kila mahali, tajiri au maskini. Inaweza ikawa ni kutoka katika chuki zisizosemwa, kuwa na manoni machache, kuwa na hoja za mara kwa mara, na hata unyanyasaji wa majumbani, na kutalakiana (itakuwa ni moja ya sababu kuu mbili kwa wanandoa kutalakiana katika taifa la Marekani). Mabishano haya hutengeneza hisia hasi kati ya wanandoa na huathiri watoto, na kufanya mambo kuwa mabaya!
- Pasipo na uratibu: wanandoa hujichukulia maamuzi au hununua vitu bila kushauriana na mwenzake jambo ambalo hupelekea upotevu fedha … na pia kusababisha mabishano; au mwenza mmoja kusimamia maswali yote ya kifedha, na iwapo mtu huyu ataondoka au kafiriki, mwenza anayebakia anakuwa hajui maswala ya kifedha ya familia, hasa kama mtu ambaye ameondoka alikuwa ni mtu pekee au mtafutaji wa vitu vyote katika familia.
- Kutoaminiana: ni swala kubwa lililojificha. Wanandoa huwa hawa aminiani katika maswala ya fedha, hutengeza chuki na kuharibu uhusiano na amani ya nyumba.
- Mitindo tofauti ya usimamizi wa fedha: ni dhahiri kuwa wanandoa wote wana mitindo tofauti ya matumizi, na tabia tofauti na maadili kutegemea historia ya maisha katika familia zao. Hivyo yawezekana umeshaanza kutekeleza kozi hii, na mwenza wako hataki kufanya ufuatiliaji, au anadhani kutengeneza bajeti ni kupoteza muda…
- Mapato tofauti: wakati mwingine mwenza mwenye kipato kidogo au hakuna hujihisi “hana maana” au mnyonge: thamani ni ya muhimu zaidi kuliko fedha inavyoweza kufanya – na mchango kwa ustawi wa familia haupimwi kwa mshahara unaopata – mwenza mwenye mshahara kidogo ama hana kabisa anaweza akawa mchangiaji mkubwa kwa ustawi wa familia.
- Matumizi mabaya ya fedha: katika kesi kubwa, mwenza mmoja wapo anakuwa na nguvu kifedha (kipato, maamuzi katika matumizi) na kuitumia vibaya kumwinea mwenzake.
Zoezi la Nyumbani:
Je, hiki ni kitu cha kawaida kwako? Kabla haujaenda katika sehemu ya pili, kagua hali ya kifedha ya familia yako – na si dolla unazopata, lakini ujuzi wako:
- Ni nani hufanya maamuzi ya kifedha?
- Je, una mwamini mwenzi wako?
- Je, huwa mnabishana juu ya fedha?
- Huwa mnabishania nini?
Kila mwenzi anaweza kufanya tathmini ya hali ya uchumi wa familia peke yake na kisha kushirikishana matokeo hayo…na kama maoni yenu yapo tofauti sana, hii itakuwa ni sehemu nzuri ya kuanza nayo! Na kama mnakubaliana juu ya ukaguzi huo, fanyeni kazi kwa pamoja ili kuboresha jinsi ya kusimamia fedha zenu kwa pamoja.
Mazoezi:
1) Haki: Haki huanzia nyumbani, hasa kwa unaowapenda na kuishi nao.
2) Mawasiliano:
-
- Unakuwa huna matumaini na fedha. Simu mpya – jambo gani hili lisilo na maana!
- Unatumia pesa nyingi kwenye vitu vya kijinga! Ni kosa lako!
- Unapenda kununua nguo mpya kila wakati!
- Unapaswa kulipia ada ya shule ndani ya miezi mitatu ijayo, tunahitaji kuweka akiba dolla 300 kila mwezi. Tunaweza kupunguza bajeti ya kwenda matembezini?
Je, unafikiri nini kuhusu sentensi hizi? Je, ni kweli halisi ama hukumu? Zinatoa maoni na kulaumu. Hatua kuu katika kujenga amani yako unapofanya majadiliano ya kifedha ni kuondokana na kuhukumu na kwenda katika kweli. Hii si rahisi kwa sababu fedha huhusisha hisia na kuzungumza na wenzi wetu ni hisia … hivyo kuzungumza na wenzi wetu kuhusu fedha ni hisia sana: kila aina ya hisia humbatana: hatia, nguvu, chuki, hofu yakushindwa kumtazama, wivu, uchoyo …
- Andaa mjadala wako: Angalia kweli zako: “Unahisi” mwenzi wako alitumia zaidi, au unahofu kuwa utashindwa kulipa kodi ya nyumba, au ungependa kumsaidia mwanafamilia. Ubongo wetu upo vizuri katika vitu vya hisia kuliko kufanya mahesabu na hii kiurahisi huharibu ukweli… hivyo tazama mara mbili hesabu zako kwanza. Kuwa chanya: jaribu kubainisha njia tofauti tofauti kadri inavyowezekana: usiwe “Tatizo” bali “suluhisho”. Kisha, weka lengo lako: unataka kupata nini toka katika mjadala huu?
- Chagua wakati sahihi: sio mara zote tunapatikana kiakili ama kihisia katika kujadili mambo magumu … hivyo usikimbilie na cha muhimu tafuta muda mzuri ambao mwenzi wako anao na akiwa katika hali nzuri.
- Wakati wa majadiliano: pumua, simamia ukweli, tabasamu, uwe mtulivu, usiwe na hasira ama kulia. Usikatae kila kitu; sikiliza na kuheshimu mawazo ya mwenzi wako. Fanyieni kazi kwa pamoja makubaliano mliyofikia – yale uliyokwisha yaandaa pamoja na yale aliyoyapendekeza mwenzi wako. Kila inapojitokeza lawama au hukumu, mrudie majadiliano yenu ili kufikia ukweli na kutafuta muafaka. Kwa kuelekeza nguvu katika ukweli kunasaidia kwenda zaidi ya hisia na kujenga mjadala wenye manufaa ambao utasaidia kupata ufumbuzi. Kama majadiliano yatakuwa ya hisia sana, acha na tafuta muda muafaka hapo baadaye.
- Imarisha mawasiliano mazuri: jambo la kusikitisha katika baadhi ya familia, fedha ni jambo kuu … na mada pekee. Jenga mazingira ya amani na yenye chachu ambapo mawasiliano juu ya mada zingine yatathaminiwa na kufurahiwa katika wakati ufaao. Hii pia itarahisisha majadiliano ya kifedha.
3) Ushirikiano:
- Weka mfano: kama husimamii vyema fedha zako, usitegemee wengine kufanya hivyo. Nenda nyuma katika masomo mengine saba ya kwanza na unayatekeleze kwa ufasaha katika maisha yako kadiri uwezavyo.
- Gawanya kazi na mzigo: Jadili namna ya kugawana matumizi (nani analipa nini – hakikisha kila mwenzi anabeba bili mojawapo kwa jina lake kama ushuhuda wa utambulisho). Chukua “mtaalamu” mhusishe katika usimamizi wa fedha kama mfanyakazi mwenzako anavyopewa jukumu katika kikozi na wote wanawajibika kwake. Hii pia inaweza tengeneza mfano bora kwa watoto wako, na baadaye pindi watakapoolewa. Kama mtu ni mzuri katika mahesabu na zana za mahesabu, mpatie kusimamia bajeti. Ama kama mtu ana muda zaidi, mpe kusimamia ufuatiliaji wa matumizi na bili (malipo, kuzitunza katika mafaili) yeye mwenyewe.
- Fuatilia ili kuhakikisha kuwa nyote mpo katika ukurasa mmoja na kuondoa hali ya kutokuaminiana. Kufuatilia gharama za matumizi ni njia bora ya kupunguza matatizo ya mabishano kwa kuzingatia dhahania: simama katika ukweli.
- Shirikisha taarifa: tenga wakati ambapo mtashirikishana taarifa na ni muhimu maamuzi kuchukuliwa kwa pamoja. Fanya maamuzi ya kukutana hata mara moja kila mwezi ili kuangalia vipaumbele vya matumizi na kufanya tathmini ya bajeti ya familia yenu. Kama kuna baadhi ya matumizi binafsi usiyotaka kuyaweka wazi (kwa mfano unaweka akiba kwa ajili ya mradi binafsi), amua itatoka sehemu gani ya bajeti ya familia na kipi kimetunzwa kama bajeti binafsi. Hakikisha kuwa mfumo wako wa uwekaji kumbukumbu (mahali ambapo nyaraka zako muhimu zipo) ni wazi na hupatikana kwa wote wawili.
- Amua pamoja: fanyeni kwa pamoja katika malengo na bajeti. Jadilianeni namna ya kufikia malengo. Wekeni vipaumbele katika matumizi kama familia.
3) Wosia
Kuwa mtu mwema kwa familia yako: Andaa kile hakuna mtu awezae kukiepuka: kufariki dunia.
- Weka nyaraka zako katika utaratibu: kuwa na nyaraka zinazothibitisha umiliki wa mali zako zote muhimu (ardhi, nyumba, akaunti za benki, uwekezaji, amana katika biashara…) pamoja na nyaraka za madeni yako yote kama yapo…na hata yaliyo madogo zaidi. Mwambie mwenza wako mahali zilipo. Ziweke mahali salama (kama vile vyeti vya masomo, vyeti vya kuzaliwa …). Unaweza pia ukaziweka katika vifaa vya kielekitroniki sehemu tofauti (na salama) eneo (iwapo nyumba yako itharibiwa). Unapokuwa katika majonzi pindi mwenza mmoja anapofariki huwa ni mbaya zaidi kwa aliyeachwa hai kujitahidi kuthibitisha kuwa walikuwa wanamiliki nyumba, au kufahamu madeni ambayo hawakuyafahamu, au nyaraka zilizoachwa hazieleweki. Mbali na hilo, katika wakati huu mgumu, ubongo unaweza kushindwa kuchukua maamuzi ya busara na pia anaweza kuwa mwathirika wa “wema” wa wasaidizi ambao watafaidika na hali hiyo na na kuvuna matunda hayo.
- Andaa wosia: pitia sheria ya taifa ya urithi na kuangalia kile kinacho takiwa kwa mwenzi wako kisheria (namna gani mali na madeni yako yatashughulikiwa, mali za kawaida za mwenzi na zile za binafsi, kipi mwenzi wako atarithi kisheria). Kama wewe ndiye mtafutaji wa mkate wa kila siku, fikiria ni jinsi gani mwenzi wako (na watoto unaowahudumia) wataishije kifedha bila msaada wako na kutambua suluhisho. Andika wosia wako ipasavyo na uutunze mahali salama ambapo inaweza patikana kwa urahisi (na mwanasheria, ama au rafiki anaye aminika au ndugu …).
- Jadili visivyozuilika: katika mambo yote ambayo hutokea kwetu, kifo pekee ndicho tulicho na uhakika nacho – lakini ndicho kitu ambacho hakijadiliwi mara kwa mara. Hivyo jaribu kujadili kwa busara bila mijadala ya kihisia na weka katika kumbukumbu na nini cha kufanywa na, mwenzi wako, angalau mara moja, kisha boresha nyaraka kila kunapohitajika.
mpango mkakati:
- Jadiliana na mwenzi wako jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika maswala ya fedha ndani ya familia (andaa mjadala wenu kwanza)
- Orodhesha malengo yenu ya familia kwa pamoja, kisha andika na mjadiliane bajeti ya familia yenu
- Tafuta njia bora kushirikishana taarifa muhimu na nyaraka
- Hakikisha kuwa nyaraka zako zote muhimu zimewekwa katika hali ya utaratibu mzuri (hasa nyaraka za mali, mikataba ya madeni…) na kwa pamoja wewe na mwenzi wako mfahamu zilipo. Hakikisha unaziboresha kila inapohitajika. Kuwa na mtu wa tatu mnayemwamini – ziweke katika mfumo wa kielekitroniki.
- Andika wosia wako