Kaa mbali na matatizo! Ni rahisi sana kuyumbishwa na kupelekea kuweka vipaumbele visivyo sahihi. Hakikisha unaweka kiasi cha kutosha kwa ajili ya vitu vyako vya lazima kwa kuweka kikomo cha matumizi.
Hili ni somo letu la nne, hivyo kama utafuatilia masomo haya kila wiki, ufuatiliaji wako lazima ujumuishe mwezi mmoja wa mapato na matumizi yako. Je, kuna mshangao wowote? Je, umeanza kujionea unatumia zaidi katika kitu gani?
Pia unapaswa kuorodesha gharama za matumizi yako ya muda mrefu (yale ambavyo huwa tupenda kuyasahau!) pamoja na madeni yako. Utaona ni tarakimu nyingi? Na ni orodha ndefu pia?
Usikate tamaa! Kama huwezi kusimamia fedha zako, wengine watakufanyia: wenye maduka, wakopeshaji, wanafamilia, marafiki …na katika kufuatilia haya yote tazama orodha hii:
- Tambua nini kinaendelea (kama hujui tatizo, huwezi pata suluhu yake!),
- Zingatia mambo yaliyo muhimu, hii ni kwa sababu pesa….ni kati ya uchaguzi na maamuzi. Na mara nyingi kuna uchaguzi wa aina nyingi! Je, tutawezaje kuchukua maaamuzi bora zaidi? Zingatia mambo yaliyo muhimu, kwa kuweka kipaumbele. Kwa mfano, wakati ukisafiri, unabeba kilicho cha muhimu tu. Na hii ni sawa na fedha.
Gharama za matumizi hazifanani: kwa kuchambua gharama za matumizi kulingana na aina zake itakusaidi kuchagua vyema. Kati ya mahitaji na matamanio? sawa, chakula ni hitaji la msingi… lakini je milo mitano ni hitaji la msingi? Na je, vipi kuhusiana na kupamba kitabu kwa ajili ya mtoto? Inawezekana ikawa ni tamanio ikiwa ni la kila siku, na je ikiwa ni zawadi ambayo imetolewa kwa mwaka? Umepanga nyumba yenye vyumba kumi: je nyumba ni hitaji la msingi ama tamanio? Na je kuhusu simu za mkononi na komputa? Ni hitaji la msingi ama tamanio? Ni vigumu kutofautisha kati ya mahitaji ya msingi na matamanio na haitoshi kabisa kukufanya ufanye maamuzi yenye ufanisi.
Hebu tujaribu kupambanua gharama za matumizi tofauti tofauti: Matumizi ambayo unaweza kuyapangilia (Kuyafanyia maamuzi)… na yale usiyoweza kuyafanyia maamuzi na hii ni kwasababu tayari umesha weka nia ya kuyatimiza kwa watu wengine: Hii ni kama vile kodi ya pango, rejesho la mkopo, bili, gharama za simu, nk … kiasi chochote ulicho weka nia ama ahidi kukilipa. Matumizi uliyoyawekea nia ama ahidi ni lazima kuyawekea kipaumbele cha kwanza hata kama kuna jambo jingine linalokupasa ulifanye bila kukosa (hata kama ni tatizo kubwa limetokea nyumbani, gharama za simu kupanda sana….), ni lazima ulipe kwani usipofanya vile ahadi ama matumizi ya lazima hupelekea kuwa na madeni.
Mpango wa utekelezaji:
Usibebe jukumu usiloweza kulimudu maana yake usije ahidi usichoweza kukitimiza, hivyo ni vyema ukafanya mahesabu vizuri kama “utaweza” lisije likakufanya ulemewe.
Ukomo wa Matumizi: Chukua orodha ya matumizi yako ya baadaye, na kisha jumlisha pamoja na ahadi ama matumizi yako yote ya lazima katika mwezi. (Kama baadhi ni ya kila mwaka, yagawe kwa 12). Toa gharama zote za matumizi yako ya mwezi katika mapato yako ya mwezi husika. Kiasi kitakachobakia ndicho utakachoweza kukipangia matumizi yake. Kisha kigawe kwa siku 30, na hii itakuonesha ni kiasi gani unaweza kutumia katika maisha ya kila siku: na hicho ndicho kikomo cha matumizi yako ya siku. Na kama utatumia zaidi ya hicho ina maana unatumia gharama za matumizi mengine uliyoahidi na mwishoe utaingia katika matatizo.
Mazoezi :
Kikomo cha matumizi ya siku hukusaidia kujisimamia na kujua ni kiasi gani unaweza kutumia … na wakati gani unapaswa kuacha. Je, umeshakwisha orodhesha gharama za matumizi yako ya baadaye? Hebu tujaribu kulifanyia kazi.
Ikiwa kipato chako ni cha kila mwezi:
- Jumlisha gharama za matumizi yako yote ya lazima pamoja na ahadi zote kwa mwezi. (kwa mfano: Kama kuna gharama moja wapo ni ya mwaka, igawe kwa 12).
- Toa gharama za matumizi yako yote katika mshahara wako wa mwezi. Kilichobakia…. ndicho utapaswa kukitumia utakavyo, katika maisha yako ya kila siku pamoja na matumizi mengine ikiwa na kuweka akiba kwa ajili ya miradi yako ya baadaye.
- Gawanya kwa siku 30…na hicho ndicho utakachotumia kila siku. Unaweza hata kwenda mbali zaidi kwa kujiwekea kiwango cha kuweka akiba kwa ajili ya miradi ama malengo yako.
Hebu tuchukue mfano huu (tarakimu hueleza kwa urahisi – zinaweza zikawa fedha zozote zile):
| |
Kiwango |
Kiasi |
Kwa mwezi |
| Kipato |
Kwa mwezi |
400 |
400 |
| Bili ya Umeme |
Kwa mwezi |
25 |
25 |
| Kodi ya pango |
Kila robo mwaka |
120 |
120/3 = 40 |
| Ada ya shule |
Mara mbili kwa mwaka |
180 |
180/6 = 30 |
| Kodi ya mapato |
Kwa mwaka |
60 |
60/12 = 5 |
| |
Jumla ya Matumizi ya lazima (kwa mwei mmoja) |
|
100 |
| |
Kipato – Jumla ya Matumizi ya lazima |
|
400 – 100 = 300 |
| |
Ukomo wa Matumizi kwa Siku |
|
300/ 30 siku = 10 |
Kwa kawaida huwa tunakumbuka mishahara yetu ya kila mwezi… hata hivyo ni makosa sana kuweka hili katika akili zetu. Kwani tayari sehemu ya mishahara yetu inakuwa imeshakwisha tumika kwenye matumizi ya lazima. Hivyo kwa kukumbuka kikomo chetu cha matumizi kwa siku inatoa kiashiria chema zaidi.
Kama kikomo cha matumizi kwa siku hakitoshi, pitia matumizi yako yote na bainisha yapi unapaswa kuyapunguza. Bakisha tu unayoweza kuyamudu.
Tumia ukomo wa matumizi ya lazima kujua kama utaweza kuhimili matumizi mengine ya lazima kabla haujaingiza mengine. Hebu tuangalie mfano hapo juu: Unataka kahamia katika nyumba nyingine na kodi yake ni 210 kwa robo mwaka (yaani kila baada ya miezi 3). Hivyo 210/3=70…maana yake ni 70-40=30 ambapo kiasi hiki kitahitajika kila mwezi. Hivyo chukua kipato chako chote toa matumizi yako ya lazima (ahadi zote)= 300-30 (kodi ya nyumba iliyoongezeka)=270 na uigawe kwa siku 30 za mwezi = 9 (kikomo cha matumizi kwa siku). Je, inawezekana kweli kuishi kwa gharama ya 9 kwa siku na ukafanya mambo ama miradi yako mingine?
Ikiwa kipato chako ni cha mwaka:
Ukomo wa matumizi kwa siku husaidia pia ikiwa unapata kipato kikubwa mara moja katika mwaka.
| |
Kiwango |
Kiasi |
Kwa mwaka |
| Kipato |
Kwa mwaka |
4400 |
4400 |
| Bili ya Umeme |
Kwa mwezi |
25 |
25 x 12 = 300 |
| Kodi ya pango |
Kila robo mwaka |
120 |
120 x 4 = 480 |
| Ada ya shule |
Mara 2 kwa mwaka |
180 |
180 x 2 = 360 |
| Kodi ya mapato |
Kwa mwaka |
660 |
660 |
| |
Jumla ya Matumizi ya lazima (kwa mwaka 1) |
|
1800 |
| |
Kipato – Jumla ya Matumizi ya lazima |
|
4400 – 1800 = 2600 |
| |
Ukomo wa Matumizi kwa Siku |
|
2600/ 365 siku = 7 |
Mara hii fanya mahesabu ya gharama za matumizi yote ya lazima kwa mwaka mmoja (hivyo, kama una bili ya kila mwezi izidishe kwa miezi 12. Ukiwa na pesa hutia majaribuni kutumia kiasi kikubwa katika jambo fulani, hivyo kwa kuweka pembeni matumizi ya lazima na kufanya mahesabu juu ya kile utakachotumia kwa uhalisia ni muhimu zaidi.
Ikiwa kipato chako hakilingani:
Ukomo wa matumizi kwa siku hufaa sana katika mapato ya mwezi ama kwa mapato ambayo yanalingana. Kingelitokea nini ikiwa unapata kipato mara kwa mara? Kama unapata kila siku, yakupasa ufanye mahesabu uone ni kiasi gani utatenga kwa ajili ya gharama za matumizi ya lazima katika siku moja. Na kama utapata zaidi, weka pembeni (Mfano katika Benki) vivyo hivyo upatapo kiasi kidogo, jaribu kuweka kiasi cha kutosha wakati tu upatapo kiasi kikubwa itakusaidia katika siku ambayo utapata kiasi kidogo.
Mfano:
| |
Kiwango |
Kiasi |
Kwa siku |
| Bili ya Umeme |
Kwa mwezi |
30 |
30 / 30 = 1 |
| Kodi ya pango |
Kila robo mwaka |
180 |
180 / 90 = 2 |
| Ada ya shule |
Mara 2 kwa mwaka |
180 |
180 / 180 = 1 |
| |
Jumla ya Matumizi ya lazima |
|
4 |
| Kodi ya mapato |
Kwa mwaka |
Asilimia 10 |
10% |
Mfano: Kwa wiki:
| |
Jumapili |
Jumatatu |
Jumanne |
Jumatano |
Alhamisi |
Ijumaa |
Jumamosi |
| Kipato kwa Siku |
10 |
20 |
0 |
10 |
50 |
30 |
10 |
| Matumizi ya lazima |
4 |
4 |
0 |
4 |
20 |
4 |
4 |
| Kodi ya mapato aslimia 10 |
1 |
2 |
0 |
1 |
5 |
3 |
1 |
| Matumizi ya Kila siku |
5 |
14 |
0 |
5 |
25 |
23 |
5 |
Katika mfano huu, mwishoni mwa wiki, tunapaswa kuweka pembeni 4 + 4 + 4 + 20 + 4 + 4 = 40 kwa ajili ya gharama za matumizi ya lazima, yaani katika siku 10. Na pia lazima kuweka kwa ajili ya kodi ya mapato kwa kila kipato tunachopata. Ni sawa na kuweka akiba ya maji wakati wa ukame ama kama vile ndege ambavyo hujiwekea akiba ya chakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Mpango wa utekelezaji: Fanya mahesabu ya ukomo wa matumizi yako. Pakua faili hili hapo chini linaweza kukusaidia zaidi. Na kama una maswali waweza uliza kwa kuingia katika uwanja wa maswali ama kwa kutuma ujumbe.