Je, bado unaendelea kufuatilia mapato na matumizi yako? Je, gharama za matumizi yako zinalingana na kipato chako? Je, umeshaorodhesha gharama za matumizi yako ya muda mrefu? Ukifikiria juu ya gharama za matumizi yako ya baadaye ni sawa na kuangalia mbele…maana inakusaidia kuona tatizo kabla halijatokea. Hebu linganisha taswira hizi mbili:
Kuzingatia uwiano wa mapato na matumizi yetu inaweza ikawa ngumu sana ikiwa tuna matumizi zaidi na wakati huo huo kipato chetu ni kidogo kabisa kuyamudu.
Nini hutokea ikiwa tunashindwa kuzingatia uwiano huo?… kushindwa kuzingatia uwiano huu…hupelekea kukopa, yaani kuwa na deni, na hii ni kwasababu matumizi yetu ni makubwa kuliko vipato vyetu, hivyo ili uweze kugharamia matumizi hayo itahitajika fedha ya ziada mbali na iliyopo. Na unapochukua mkopo/deni utambue kuwa unatumia kipato chako cha kesho.
Hebu fikiria kipato chako ni keki. Na leo keki yako haitoshi … hivyo unaamua kuazima kipande kimoja cha keki cha ziada.
Utahitajika kukirudisha kipande hicho kesho yake. Na je, utawezaje kukilipa? Ukizingatia fedha ulizo nazo hazitoshi: yakiwemo mapato ama akiba yako pia haitoshi. Hivyo itakupasa kesho yake ule pungufu kwani kipande kimoja cha keki kitahitajika kufidia ulichokopa.
Deni la leo ni kutumia kipato chako cha kesho. Ikiwa vipato vyetu vitaongeza tunaweza kuyamudu madeni yetu… lakini madeni huwa kama ndoto za abunuasi, endapo 1) Mapato yetu yapo imara, au yanasuasua, ama yanashuka, 2) Pindi deni linapozidi kuongezeka kwa sababu ya riba, 3) Wakati gharama zingine zisizotarajiwa kutafuna vipato vyetu. Madeni mara zote hutuletea shida katika siku za baadae…hivyo ni vyema ufikirie kwanza namna ya kulipa deni hilo kabla ya kukopa.
Madeni yasiyolipwa kwa wakati hukua:
Hili ni somo lefu sana leo – tutaangalia zaidi juu ya riba. Riba ni kanuni ambazo wanadamu wamejiwekea na hupelekea “deni” kukua baada ya muda fulani. Hivyo, mfano mimi nakopa dolla 100… itanipasa baadae kurejesha dolla 101 au dolla 110 ama dolla 106…hii ni kutegemeana na kiwango cha riba kilichowekwa. Kama unachukua mkopo tambua kuwa riba mara nyingi hupelekea shida katika siku za baadae, 1)Kabla ya kukopa fikiria namna utakavyolipa, 2)Jaribu kutafuta mbadala wowote au mkopo usiokuwa na riba.
Jambo moja zaidi la kuwa makini nalo ni kuwa, madeni yasiyolipwa kwa wakati hukua haraka. Riba ni kama magugu, au panya … Kama huwafukuzi (hulipi madeni), huendelea kuongezeka au kuzaliana … na kwa muda mfupi sana panya watakuwa wamezagaa katika nyumba yako yote.
Kwa nini? Hii ni kwasababu riba isiyolipwa kwa wakati hupelekea kuwa deni, na hupelekea kuengezeka kwa riba zaidi na zaidi, hivyo usipolipa madeni yako kwa wakati, yataendelea kukua mara dufu. Madeni yasiyolipwa kwa wakati hukua haraka sana.
Kazi ya nyumbani: Orodhesha madeni yako yote na hakikisha kuwa umeyaandika na kusainiwa kati yako na mkopeshaji.
Maoezi:
Kazi ya nyumbani: Orodhesha madeni yako yote. Madeni yasiyoandikwa na kusimamiwa vizuri ni mabaya mno. Kwani yanafananishwa na moto. Manufaa ya Moto yanaweza kuwa ni kupikia na kupasha joto…lakini kama hautakuwa mwangalifu, moto unaweza unguza nyumba yako.
Ndivyo ilivyo kwa madeni: usikubali madeni yaharibu mapato yako.
1) Orodhesha madeni yako yote – hata yahusuyo familia, na yaliyo madogo (madeni yasiyolipwa ama “yaliyosahaulika” yanaweza kuchochea chuki baina ya watu…): kiasi, tarehe, kiasi ulichokwisha lipa, kiasi unachodaiwa, awamu za kulipa (yaani kiasi unacholipa – mara ngapi na ni kiasi gani), na kuonyesha kama riba inaongezeka ama la! Na kama haufahamu vizuri baadhi ya madeni yako, haujachelewa bado kuyapambanua – kwa kawaida kama haujaweza kupambanua mambo (hasa maswala ya fedha) hautaweza kupata usahihi wake kwa wakati…na itakupa shida kuyaelewa. Hivyo rekebisha orodha uliyonayo.
Kwa kawaida orodha hii itakuwa na manufaa sana wakati (katika masomo machache) wa kupangilia kiasi kidogo tulichonacho kama kitu kimoja na kuweka mipango ya baadae (bajeti).
2) Wengi wetu hatupendi hisabati…lakini kama unaweza, jaribu kuelewa mahesabu juu ya riba. Hebu tuchukue mfano huu mdogo: Unakopa dolla 1000 wakati huo huo riba yake ni asilimia 10 – ikimaanisha “katika kila 100” kuna ongezeko la dolla 10. Swali la awali kabisa la kujiuliza ni kuwa, hii riba ya asilimia 10 ni ya kila mwaka, kila mwezi, kila wiki—ama kila siku? (Unatakiwa kupambanua hilo). Hebu tuseme ni ya kila mwezi.
Na baada ya mwezi mmoja, utakuwa unadaiwa kiasi gani?
Hebu tuseme kwamba…:(huna fedha). Unaamua kujadiliana na mkopeshaji ambaye yupo tayari kukuongezea muda wa mwezi mmoja zaidi wa kulipa mkopo wako. Hivyo, itakupasa ufikirie ni kiasi gani utalipa mwishoni mwa mwezi wa pili?
Maswali? Weka katika jukwaa letu la maswali.