Watu wazima hufanya … watoto hujifunza: jinsi ya kulea watoto wenye kuwajibika kifedha.
Je, umekwishaanza kuzungumza na mwenzi wako kuhusu masawala ya fedha? Mmepata njia ya kufanya kazi kwa pamoja katika kupanga, vipaumbele katika matumizi na maamuzi? Hebu tuongeze uwanda wa mjadala na tuone jinsi gani tunaweza kuwaelimisha watoto wetu kuhusu maswala ya fedha. Hata kama wewe si mama au baba, fikiria juu ya watoto wengine unaoweza kuwashawishi: wapwa zako, binamu, wadogo zako, watoto wa majirani, na vijana unaowafundisha…
… Bila ya kutambua hilo, tayari utakauwa umeshawaelimisha. Namna gani? Watoto hujifunza mengi zaidi kwa kuangalia yale watu wazima hufanya na kutenda … kuliko kwa kusikiliza maneno … hasa wakati tunapofanya kile tunachokisema! Jiangalie mwenyewe! Jiweke katika hali ya mtoto… unajifunza nini kivitendo kutoka katika hali hii kila siku?
- Wazazi wangu huwa hawasemi hapana ninapotaka kununua kitu chochote niwapo dukani.
- Huwa siwasikii wazazi wangu kujadiliana ya fedha.
- Wazazi wangu waliniahidi kiasi cha fedha fulani- kama nitapata alama nzuri shuleni.
- Wazazi wangu hufanya manunuzi na wakati mwingine humwambia mwenye duka watamlipa baadaye.
- Wazazi wangu hujadiliana juu ya matoleo ya vifaa vipya vya kielekitroniki na fasheni zingine ambazo marafiki zao wamenunua na katika muda kidogo na wao wananunua pia.
Tunafanya, wanatuelewa
| Kile tunachokifanya |
Kile watoto wetu wanakielewa |
| Huwa hatukatai pindi watoto wetu wanapotaka kununua kitu chochote wawapo dukani. |
Fedha haziishi. |
| Hatuzungumzii maswala ya pesa. |
Pesa ina mihujiza yake. |
| Tumewaahidi watoto wengi kiasi cha pesa fulani wanapofanya vizuri shuleni. |
Lengo la kujifunza ni kuelewa mambo mengi. |
| Mara nyingine huwa tunafanya manunuzi na kumwambia muuzaji kuwa tutamlipa baadaye. |
Haikatazwi kuwa na madeni. |
| Huwa tunazungumza juu ya matoleo mapya ya vifaa vya kielekitroniki au fasheni ambazo marafiki zetu wamenunua na katika kipindi kifupi na sisi tunavinunua pia. |
Kitu kipya ni bora. Dunia haina kikomo cha rasilimali. |
Mpango mkakati:
- Jichunguzeni wenyewe kwa siku chache … Mnafanyia nini pesa zenu, nini hamfanyi, na mvae viatu vya mtoto: wanaelewa nini?
- Tumia mbinu nyingine tofauti: orodhesha kile ungependa watoto wako (au watoto wanaokuzunguka) waelewe kuhusu fedha … Orodhesha maadili (uaminifu, uvumilivu, uwajibikaji, ukarimu, nk …) ambayo ungependa watoto kuyafuata –jadiliana maadili haya na mwenza wako.
- Bainisha mazingira halisi ambapo watoto wako wanaweza kuangalia jinsi unavyotekeleza maadili hayo kwa vitendo.
Mazoezi
Soma baadhi ya mapendekezo :
Usiache watoto wako waharibiwe na fedha. Wamejifunza kutazama video wakati wakitembea? Ama kuandika? Hawawezi kujifunza maswala ya fedha kwa kusoma kitabu cha fedha wakiwa na miaka 20…wanahitajika kufanyia zoezi, kufanya makosa na majaribio!
Waelimishe kwa kuwapa nafasi ya kusimamia fedha na kubeba majukumu wanapoendelea kukua. Kwa kuwapa tabia nzuri na mfumo bora wa kimaadili ndilo jukumu letu kuu kama wazazi: Iwe ni chakula, usalama, usafi, mahusiano ya kijamii … na hata fedha. Iweke fedha katika mtazamo wa kimalezi na kufanya kuwa ni hali yako ya kimaisha ya kila siku na kuwa fursa za kujifunza…. anza wakati wakiwa bado ni wadogo! Masoko na matangazo ya kibiashara “huwafunza” kuwa walaji katika umri mdogo.
Chini ya Umri wa Miaka 5:
- Kuwa thabiti: wape zawadi tu katika hafla maalum (likizo, siku za kuzaliwa, kuzaliwa kwa ndugu …).
- Sema hapana … watajifunza mengi.
- Tumia vilivyopo … usikimbilie kununua vitu vipya kila wakati.
- Nenda nao unapokwenda kufanya manunuzi na uzungumze kwa sauti unapofafanua chaguo lako: Sina haja hiki, hii haipo katika orodha yangu, hiki ni bei ghali sana, nk …
- Usichanganye vitu na upendo: yakupasa uwape (muda wako, mawazo yako): wafanye wajisikie wahimu … hiki ndicho wanahitaji.
Kati ya 6 hadi 10:
- Fuatilia matumizi yako na uandike bajeti kila wakati na na iweke mahali ambapo watoto wako wanaweza kuona kile unachokifanya. Watafahamu kuwa ufuatiliaji na bajeti ni kitu cha kawaida kufanyika.
- Wape kazi ndogo za kufanya: kununua chakula, au mambo madogo madogo: wape orodha na uwakabidhi kiasi cha fedha. Waombe wafuatilie kila walichokitumia na wakupe chenji inayobakia. Na wakizoea, waulize ni kiasi gani wanahitaji kabla hawajaununua vitu. Itawasaidia kuendeleza hali ya utambuzi wa bei. Kama watanunua vitu ambavyo haviko kwenye orodha, wauliza kwa nini. Waambie kuwa watapeleza kununulia kitu kingine (kitaje hicho kitu).
- Kama wakiomba vitu vikubwa (baiskeli …), nenda nao mkaulize bei tofauti tofauti na ili kulinganisha, ni kiasi gani mnatakiwa kuweka akiba kila mwezi kabla ya kununua baiskeli.
Miaka 12 na zaidi:
- Wahusishe katika maamuzi ya kifedha na matumizi ya kila siku kwa kuwapa majukumu ya kutekeleza kwa kutumia kiasi cha fedha za familia yako – sio fedha kwa ajili ya matumizi yao (wanaweza wakaitumia kwenye vitu visivyo vya msingi na wasi jifunze chochote) – lakini katika vitu vya muhimu ni kama vitabu vya shule, viandikia au chakula.
- Na wanapokuwa watu wazima, hatua kwa hatua jukumu la fedha linakuwa juu yao. Kwa mfano, kuamua (angalia bajeti yako kwanza) kiasi kwa ajili ya nguo zao au simu zao (kama wana moja) waache wajisimamie. Wape taratibu zinazoeleweka na wazifuate: ikiwa tayari wameshatumia bajeti ya fedha kwa ajili ya nguo…ndani ya siku mbili, ni mbaya sana – itawapasa kusubilia hadi mwezi unaofuata. Watajifunza madhara ya kutumia zaidi na kuwa pesa hazitoshelezi. Hii hapa ni mifano ya matumizi ambayo unaweza ukawabebesha watoto kuyasimamia:
- Rejerea bajeti ya shule (viandikia, vitabu …),
- Bajeti ya chakula,
- Siku kuu (Mwaka Mpya / Krismasi / Eid …),
- Zawadi kwa marafiki …
- Wape kiasi kamili (kulingana na bajeti yako) na waache waisimamie. Watajifunza jinsi ya kuchukua maamuzi na kuzingatia bajeti.
- Washirikishe katika maamuzi makubwa kama kugharamia masomo yao, jinsi inavyoathiri ndugu wengine, watie moyo kufanya kazi … lakini kusoma kuwe ni kipaumbele. Wasaidie kutambua kazi watakayoweza kuifanya.
- Kuwa mfano wa kuigwa: waonyeshe jinsi unavyo orodhesha gharama za matumizi ya baadaye, linganisha bei tofauti tofauti, na usimamie katika mpango wako.
- Tenga muda kwa ajili ya watoto wako na uwaonyeshe upendo… kwa kukosa muda usiwafurahishe kwa kuwanunulia vitu. Soma vitabu, wapeleke matembezini, cheza nao … wasikiliza – kwa ufasaha.
- Himiza maadili mema (uaminifu, kutokujivuna, uaminifu, uwajibikaji …) na mtazamo chanya kuhusu fedha: fedha ni chombo kinachotusaidia katika maisha, na si lengo. Kwa mfano, kabla ya sikukuu, jadili umuhimu wa sikukuu hiyo … ili wasiweze kudhani tu kuwa sikukuu ni mlindikano wa zawadi na pipi. Jumuisha na zawadi zisizokuwa vitu, kutoa kwa wengine …