Curriculum
Course: usimamizi wa fedha
Login
Text lesson

6. Usitembee pasipo kuwa na mwanga: Panga!

Ilikuwaje wiki yako juu ya matumizi yakinifu? Je umeshajiuliza mwenyewe “kwa nini” lini ulikwenda kufanya manunuzi? Leo, tunaweka pamoja vipande vyote kwa pamoja ili kufanya ukamilisho. 

Hebu fikiria umepotea jangwani ukiwa na chupa moja tu ya maji. Utafanya nini?  

Amua utaenda wapi, kadiria muda gani utatumia kufika mwisho wa safari yako…na panga kiasi gani cha maji utakunywa kwa kila siku.  

Hebu tusema umekadiria siku 5: Hakikisha unachora mistari mitano ili kudhibiti kiasi cha maji unayokunywa.  Mistari mitano hutengeneza sehemu sita: siku 5 jumlisha na 1 ya dharura. 
Na hii ndio maana halisi ya kupanga. 

Katika sehemu ya jangwa weka “muda” na maji weka “fedha”…tenga kipato chako katika kila gharama unazofanya. 

Usitembee pasipo kuwa na mwanga: Kama kipato chako ni cha mwezi…jaribu kupanga kwa mwezi mmoja. Na ikiwa utamudu kufanya hivyo, waweza kupanga kwa muda mrefu zaidi (Miezi 6, ama 12). 

Anzia parahisi na uende pagumu (kama kupangilia): kile unachofahamu bayana, mbali na usichokifahamu (kijumulishe pia) 

  • Pangilia matumizi yako ya lazima (kodi ya pango, bili za umeme , bili zingine, marejesho ya madeni kama yapo): na kama hazibadiliki ni rahisi zaidi, na kama sivyo angalia bili zako za nyuma na uweke makisio mazuri. 
  • Pangilia Kipato chako: mshahara wako kama umeajiriwa au makisio yako kama unafanya kazi zako mwenyewe. 
  • Fanya makisio ya gharama ya matumizi yako ya kila siku: (hii itakusaidia kufanya ufuatiliaji wa uhakika):Chakula, usafiri, usafi, starehe …
  • Weka pamoja matumizi mengine (au kipato)(au mapato) mipango ya kulipwa (kupata) katika mwezi husika: kwa mfano, baiskeli yako inahitaji tairi mpya, au ni sherehe ya kuzaliwa ya dada yako. 
  • Kisha, kumbuka kiasi ambacho unatakiwa kuweka akiba kwa ajili ya gharama za matumizi ya baadaye (Malengo na vitu vya lazima). Endelea kufanya mahesabu hadi hapo uwiano utakapopatikana.  

Fuatilia Mpango wako! Usitembee pasipo kuwa na mwanga. Kuna namna nyingi za kuhakikisha kuwa unafuata mpango wako – chagua njia inayofaa kwa ajili yako. 

  1. Akaunti ya Benki: Weka katika akaunti ya benki amana zako kwa ajili ya kulipia matumizi yako ya lazima na uweke kwa ajili ya malengo yako. Au, kwa uzuri zaidi, unaweza weka fedha zako zote katika akaunti yako ya benki na yakupasa kutoa kiasi cha pesa ambacho kitatumika kwa siku ama kwa wiki inayofuata. 
  2. Tumia Bahasha: Mfano huwa unatumia zaidi ya kile ulichokuwa umepanga, weka kiasi cha fedha katika bahasha moja ambacho umepanga kutumia kwa wiki husika na chukua bahasha hiyo tu pindi unapotaka kwenda kufanya manunuzi. Usijidanganye mwenyewe! Usichukue katika bahasha nyingine. Itakupasa kusubiri kipato kingine kujazia. 
  3. Angalia mahali ulipo: Linganisha kiuhalisia kile unachotumia (Ufuatiliaji wako) kulingana na bajeti yako: Inautofauti wowote? Rekebisha mpango wako – kwa mfano, hukupanga kufanya marekebisho ya baiskeli yako, lakini imepata pancha na ikahitajika kuibadili tairi katika mwezi huo, yakupasa kuangalia kifungu kingine katika bajeti (punguza hitaji moja ama tumia kiasi chako cha dharura au kama unafanya kazi zako mwenyewe, ongeza kipato chako). 

Endelea kupanga – kwa kufanya zaidi, itakuwa rahisi. Usitembee bila kufahamu uendako na kwa namna gani.: Usitembee pasipo kuwa na mwanga! 

Zoezi la nyumbani: Andika bajeti yako mwenyewe.

Mazoezi

Haya ni baadhi ya mawazo yatakayokusaidia kutengeneza bajeti yako na kupangilia kipato, akiba na gharama za matumizi yako. 

  1. Mchanganuo: Ili kurahisisha tumia utaratibu sawa na makundi katika kufuatilia uhalisia wa matumizi yako: angalia mstari kwa mstari: kiasi gani umepanga kupata? Tumia penseli…kwani utakuwa unabadilisha tarakimu mara kwa mara kuhakikisha inakuwa sawa.  
  2. Kompyuta: ndiyo…bajeti inahusisha tarakimu nyingi sana…hivyo ukitumia kompyuta itarahisisha zaidi(tazama mfano hapa chini) au tumia programu yoyote kwa ajili ya kufanyia mahesabu ya fedha (hasa kama unapokuwa na akaunti nyingi za benki, uwekezaji…) 
  3. Programu: kuna programu nyingi ambazo unaweza tumia kuingiza mapato na matumizi ya bajeti yako. 
  • Tulia – kwani haitakuhitaji kukimbia umbari mrefu wa kilomita 10 kama hujawahi kimbia kabla. Hautaweza kupanga miezi 12 moja kwa moja. Hivyo itakupasa kufanya hatua kwa hatua. Panga kwa ajili ya mwezi unaofuata kwanza. Usisahau kuingiza kiasi cha akiba utakachotumia kwa matumizi ya mwaka. 
  • Tafuta kiwango cha taarifa za kina: kama inaeleza kwa kina, itakuwa na tarakimu nyingi zaidi, na itakuwa vigumu kufuata na hatimaye kukata tamaa. Kusanya kiasi kilicho kidogo kama itaruhusu. Ukihitaji kuzingatia matumizi makubwa (hasa miradi ya mwaka ama zaidi, au gharama za matumizi ya lazima) hakikisha unapangia pia.  
  • Kuwa thabiti: Tumia makundi sawa kama ilivyo katika uhalisia wa ufuatiliaji wako. Ufuatiliaji hukuonesha jinsi unavyotumia, bajeti yako pia hukuonesha nini ungependa kutumia hapo baadae. Tumia makundi muhimu: kama utajumlisha malengo mengi muhimu ya muda mrefu (masomo, watoto, nyumba…) na umepanga bajeti iliyobana kwa maswala ya kijamii kwa mfano, piga mahesabu juu ya mialiko utakayoimudu katika mwezi, unaweza kununua zawadi kiasi gani, n.k

Kitu cha muhimu zaidi ni kifaa ambacho utaweza kukitumia kwa uzuri na kukusaidia kupiga mahesabu, kufuatilia bajeti yako na kuendelea kuihuisha. Usitembee pasipo kuwa na mwanga: Mpango!